News
MRADI WA TIMIZA MALENGO WAZINDULIWA. SASA KUFIKIA MIKOA 10 NA WILAYA 36
MRADI WA TIMIZA MALENGO AWAMU YA TATU WABISHA HODI MIKOA 10 YA TANZANIA BARA
Na. Mwandishi Wetu – MAELEZO, Ruangwa – Lindi .
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Hamis Nderiananga amezindua Awamu ya tatu ya mradi wa Timiza Malengo chini ya kampeni Tusonge na Samia kutokomeza UKIMWI wenye lengo la kukabiliana na maambukizi mapya ya VVU miongoni mwa vijana nchini.
Akizindua mradi huo Februari 20, 2025 wilayani Ruangwa mkoani Lindi, Mhe. Ummy amesema Serikali imeweka mikakati madhubuti ya kupambana na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI nchini miongoni mwa vijana akibainisha kuwa Serikali kupitia Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania(TACAIDS) ilianzisha mradi huo mwaka 2018 ili kuwajengea uwezo vijana kukabiliana na changamoto zinazowapelekea kupata maambukizi ya VVU.
Amesema mradi huo tangu kuanzishwa kwake umeonesha mafanikiomakubwaambapo katika awamu ya tatu vijana wa kike na kiume wa mikoa 10 na Halmashauri 36 watanufaika. Mikoa hiyo ni pamoja na Dodoma, Singida, Morogoro, Tabora, Mara, Tanga, Geita, Ruvuma, Njombe na Lindi.
“Tumekutana katika tukio hili la uzinduzi wa Awamu ya Tatu ya Mradi wa Timiza Malengo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Kampeni ya TUSONGE NA SAMIA KUTOKOMEZA UKIMWI ambayo ni hatua muhimu ya kuhakikisha vijana wa Tanzania wanakua na afya njema na uwezo wa kutimiza ndoto zao na majukumu yao katika jamii “.Amesema Mhe. Nderiananga.
Amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kukabiliana na magonjwa mbalimbali nchini ikiwemo kupungua kwa maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI”
Amesema katika kuhakikisha maambukizi ya Virusi vya UKIMWI yanapungua nchini TACAIDS imeanzisha kampeni inayoitwa TUSONGE NA SAMIA KUTOKOMEZA UKIMWI kwa kutambua juhudi na mchango wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutokomeza UKIMWI ambapo kupitia uongozi wake yamefanyika maboresho makubwa ya huduma za kinga, tiba na matunzo kwa Watu wanaoishi na VVU (WAVIU).
Ameongezakuwa awamu ya Tatu ya Mradi wa Timiza Malengo imeongeza wigo wa kuwafikia vijana balehe wa kiume ambao watapatiwa Mafunzo na wataunganishwa na vijana wa kike na taasisi zinazotoa huduma za kiuchumi zenye masharti nafuu, Taasisi zinazotoa mafunzo ya uanagenzi, VETA, Kilimo na Mifugo.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba ameeleza kuwa Serikali imeweka vipaumbele mahususi vya kuwahudumia Vijana kama mkakati wa kupunguza maambukizi ya VVU ikiwemo kutoa elimu sahihi kwa Vijana dhidi ya kujikinga na VVU na UKIMWI, kuwezesha upatikanaji wa huduma nafuu kwa makundi ya vijana kuwapa maarifa na ujuzi wa kutumia fursa za maendeleo zilizo katika maeneo yao.
Amesemamradi wa Timiza Malengo ni fursa nzuri ya kuwafikia vijana wengi zaidi kwa kuwapa ujuzi na maarifa ya kujiendeleza kiuchumi pia kukabiliana na maambukizi mapya ya VVU, kuwaendeleza vijana kielimu pia kuwashirikisha vijana kwenye majukwaa ya maamuzi ili waweze kushiriki katika kupanga na kuweka mikakati yenye lengo kupunguza maambukizi ya VVU.
"Mradi huu unalenga kuwaelimisha vijana wajitambue na kujilinda na changamoto zinazopelekeatabia hatarishi zinazopelekea maambukizi ya mapya ya VVU. Nawapongeza Watendaji wote kwenye mradi huu pia nawashukuru watumishi wote wa Ofisi ya Rais -TAMISEMI walioko kwenye Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kutoka mikoa 10 na Halmashauri 36 Kwa utayari wenu wa kusimamia mradi huu ili uendelee kuleta tija kwa vijana".
Amesema Serikali imeendelea kuimarishaSekta ya afya ya msingi inayotegemewa na wananchi kwa asilimia 75 kwa kufanyauwekezaji wa zaidi ya shilingi trilioni 1.29 ndani ya miaka 4.
Aidha, katika hatua nyingineameeleza kuwa Serikali imejenga na kufanya ukarabati wa Hospitali, vituo vya afya na Zahanati kote nchini.
"Katika kipindi cha miaka 4 ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan bajeti ya dawa imeongezeka kupitia Bohari ya Dawa ( MSD) kutoka bilioni 96 mpaka bilioni 116 piaametoa ajira zawatumishi wa Kada yaafya 25,936 ili kuimarisha utoaji wa huduma katika maeneo ya kutolea huduma za afya.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Catherine Joachim ameeleza kuwataatifa ya utafiti wamwenendo wa VVU na UKIMWI mwaka 2023 inaonesha kuwa Watanzania kati ya 1,548,000 hadi 1,700,000 wanaishi na VVU akibainisha kuwatakribani watu 60,000 wanapata maambukizi mapya ya VVU kila mwaka ikilinganishwa na watu 72,000 ambao walipata maambuki kwa mwaka 2015/2016.
Amesemakiwango cha maambukizi ya VVU katika mikoa ya Njombe, Songwe, Mara, Mbeya, Lindi,Arusha na Mtwara kimeongeza. Aidha, kiwango cha maambukizi ya VVU katika makundi maalumu ya Wanawake wanaofanya biashara ya ngono, jamii inayozunguka migodi, mialo ya wavuvi, madereva wa magari ya masafa marefu na Vijana bado hakijapungua.
Kwa upande wa vifo vitokanavyo na UKIMWI ameeleza kuwa Takwimu zinaonesha kuwa watu 18,000 walifariki mwaka 2023 ikilinganishwa na watu 31,226 waliofariki kutokana na UKIMWI mwaka 2018.
***Mwisho***