Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania
The Prime Minister's Office

Tanzania Commission for AIDS

Tanzania Commission for AIDS

News

TACAIDS imeandaa Kampeni harakishi ya kutokomeza UKIMWI ifikapo 2030


Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dkt. Catherine Joachim amesema TACAIDS imejipanga kutokomeza UKIMWI ifikapo mwaka 2030. Hayo yamesemwa katika kikao cha Watumishi wa TACAIDS kilichofanyika leo jijini Dodoma kwa lengo la kuboresha utendaji wa Taasisi hiyo.

Dkt Catherine ameeleza kwamba, Utafiti wa mwenendo wa UKIMWI wa 2022/23, umeonyesha maambukizi ya VVU yamepungua kutoka watu 72,000 (2016/17) kwa mwaka hadi watu 60,000 kwa mwaka. Kiwango kikubwa cha maambukizi kiko kwa vijana haswa wa kike.

Ili kupunguza maambukizi mapya ya VVU na kufikia azma ya kutokomeza UKIMWI ifikapo 2030, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji amesema kuwa TACAIDS imeandaa Kampeni ya Tusonge na Samia kutokomeza UKIMWI. Kampeni hii imepanga kutoa Elimu kwa umma hususani vijana na makundi ya jamii yanayochochea maambukizi ya VVU pamoja na kufanya uraghibishi wa Matokeo ya Utafiti Mwenendo wa Viashiria vya VVU /UKIMWI ( 2022/2023) kwa viongozi wa Tawala Za Mikoa na Serikali Za Mitaa.

Kampeni hii inalenga kuwa na uendelevu katika mwitikio wa UKIMWI na kuongeza kasi ya kufikia malengo ya kutokomeza UKIMWI ifikapo 2030.