News
TACAIDS YARATIBU UTOAJI WA MAFUNZO YA VVU NA UKIMWI VIWANDANI - JIJINI DODOMA
Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania - TACAIDS kwa kushirikiana na wadau wa UKIMWIwametoa elimu kwa wananchi wa kata ya Viwandani jijini Dodoma kuhusu kujikinga na maambukizi ya VVU, matumizi sahihi ya Kondom, kupinga ubaguzi na unyanyapaa kwa Watu Wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI (WAVIU) na namna yakuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa Mtoto
Utoaji huo wa elimu umeambatana na zoezi la upimaji wa VVU kwa hiari ambapo Jumla ya watu 16 wameweza kupima ikiwemo wanawake 5 na wanaume 11 na jumla wa watu 53 wamepatiwa vipimo vya jipime (Self-test kit).
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mratibu anaesimamia Afua za UKIMWI katika sekta za umma kutoka TACAIDS Dkt. Hafidh Ameir alisisitiza kuwa vijana ni kundi muhimu katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI, hivyo ni lazima waongezewe maarifa ya kujikinga na VVU, kuhamasishwa waweze kupima ikiwa ni pamoja na kufikia huduma za tib ana matunzo.
Aidha, ameeleza kuwa mafunzo haya ni sehemu ya jitihada za kitaifa za kufikia lengo la kudhibiti maambukizi mapya ya VVU ifikapo mwaka 2030.
Kwa upande wao, washiriki wa mafunzo wameelezeakufurahishwa na elimu waliyoipata na kuahidi kuwa mabalozi wazuri katikakupinga unyanyapaa, Kuhamasisha wenzao kujitokeza kupima na kutumia njia salama za kujikinga dhidi ya maambukizi ya VVU.

