Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania
The Prime Minister's Office

Tanzania Commission for AIDS

Tanzania Commission for AIDS

News

ZERO DISCRIMINATION DAY


Tanzania yaadhimisha Siku ya Kupinga Unyanyapaa na Ubaguzi Dunian.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe Jenista Mhagama amesema lengo la maadhimisho ya Siku ya Unyanyapaa na Ubaguzi Duniani nikukumbushana wajibu wa kila mmoja wetu, taasisi na asasi mbalimbalikwa ajili yakupaza sauti na hivyo kupinga na kupiga marufuku vitendo vyote vya unyanyapaa naUbaguzi na kukosekanausawa na haki miongoni mwa makundi mbalimbali ya kijamii, hayo yamesemwa leo kwenye hotuba yake iliyosomwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt Jerome Kamwela.

Amesema dhana na vitendo vya Ubaguzi vinavyoashiria kutokuwepo kwa usawa vinasababisha kutotimia kwa malengo yetu ya kitaifa ya mwitikio wa VVU na UKIMWI na kurudisha nyuma jitihada za Serikali za kutokomeza UKIMWI.

Maadhimisho hayo yalibebwa na kauli mbiu isemayo Linda Afya kwa kulinda haki” inahimiza kuwa na mifumo imara ya kisheria, kiutamaduni na kijamii ili kujenga mazingira yanayopelekea uwepo wa haki katika upatikanaji nautoaji huduma bora za kiafya. Aidha amesema kauli mbiu hii inatutaka kuimarishamifumo yetukwa ajili ya kuwekausawa na kutokomezaubaguzi na unyanyapaa miongoni mwa watu wanaoishi na VVU.

Mwenyekiti wa Baraza la Watu wanaoishi na VVU (NACOPHA) Bibi Leticia Moris amesema Unyanyapaa na ubaguzi bado upo na unatishia mwamko wa jamii kutumia huduma za UKIMWI zinazotolewa na Serikali na kwa gharama kubwa na hivyo kurudisha nyuma jitihada za Serikali na wadau katika kutokomeza VVU na UKIMWI nchini.

Bi Leticia ametaja Mila potofu, imani za kidini, uelewa mdogo juu ya UKIMWI ni baadhi ya vichocheo vya unyanyapaa katika jamii zetu.

Aidha amesema kuwa kupitia ufadhili wa wadau mbalimbali wa maendeleo, Baraza linatekeleza shughuli za mwitikio wa UKIMWI ikiwa ni hatua za kuunga mkono jitihada za Serikali kufikia malengo ya 95-95-95 ifikapo 2030.

Bi Leticia ameongeza kuwa katika jitihada za kupinga unyanyapaa na ubaguzi kwa WAVIU, moja ya vipaumbele vya Baraza ni kujenga uwezo wa WAVIU katika makundi mbalimbali ngazi ya jamii, ambapo kwa sasa baraza linaratibu Mitandao ya Kitaifa mitatu kwa lengo la kuongeza wigo wa ufikiwaji wa makundi hayo katika huduma za VVU na UKIMWI, kupunguza athari za unyanyapaa na ubaguzi miongoni mwao, na kuhimiza kudumu katika ufuasi sahihi wa dawa za kufubaza VVU

Ameyataja makundi hayo kuwa ni Watu wenye Ulemavu, Wanawake na Vijana, Mtandao wa Kitaifa wa Watu wenye Ulemavu wanaoishi na VVU (NNPD+), Mtandao wa Kitaifa wa Wanawake Wanaoishi na VVU (NNW+), na Mtandao wa Kitaifa wa Vijana wanaoishi na VVU (NYP+).

Mkurugenzi Mkazi wa UNAIDS Bw. Martin Odiit amesema suala la unyanyapaa na ubaguzi ni ukiukwaji wa haki za binadamu na hivyo hauhitaji kuendelea kuwepo kwakuwa unarudisha nyuma mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.

Dkt Odiit ameongeza kuwa kuna makundi mengi yanayoathiriwa na unyanyapaa na ubaguzi yakiwemo makundi ya vijana hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha tunamaliza unyanyapaa. Aidha ameongeza kuwa UNAIDS itaendelea kutoaushirikiano katika kuhakikisha unyanyapaa na ubaguzi unamalizika.